KISARAWE 2 KUPATA UMEME MWEZI HUU

KISARAWE 2 KUPATA UMEME MWEZI HUU

Like
359
0
Tuesday, 21 April 2015
Local News

WANANCHI wa Kisarawe 2 Wilayani Temeke Jijini Dar es salaam wametakiwa kutumia Wataalamu waliosajiliwa na Shirika la Umeme Nchini- TANESCO,kufanya Wayaring katika nyumba zao ili kuondoa usumbufu wakati wa usambazaji wa huduma hiyo Majumbani.

Wito huo umetolewa na Diwani wa Kata hiyo ISSA HEMEDI ZAHOR  katika mkutano na Wananchi, wakati wa Makabidhiano ya Transfoma kwa ajili ya kusambaza umeme kwa Kata hiyo iliyotolewa na Kampuni Property International.

Diwani ZAHORO amesema kupatikana kwa kifaa hicho muhimu ni kiashirio tosha kuwa umeme utapatikana katika Kata hiyo kwa wakati kama ambavyo wamepanga.

Comments are closed.