KITUKO CHA HAKI ZA BINADAMU KIMELAANI KITENDO CHA KUPIGWA KWA MWENYEKITI WA CUF

KITUKO CHA HAKI ZA BINADAMU KIMELAANI KITENDO CHA KUPIGWA KWA MWENYEKITI WA CUF

Like
232
0
Thursday, 29 January 2015
Local News

KITUO cha sheria na haki za binadamu kimelaani vikali kitendo cha kupigwa kwa Mwenyekiti wa chama cha Wananchi –CUF, Profesa IBRAHIM LIPUMBA na kusema kuwa kitendo hicho ni cha kinyama.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini dar e s salaam Mkurugenzi wa Kituo hicho, HELLEN KIJO BISIMBA amesema kuwa kumekuwa na ubaguzi mkubwa hasa katika vyama vya siasa jambo linalopelekea kuvigawa vyama hivyo na kuvikosesha haki yao ya msingi.

Aidha amesema kuwa kitendo cha jeshi la polisi kujichukulia sheria mkononi kwa kumpiga kiongozi huyo na waandishi wa habari ni kitendo cha kulaaniwa hivyo amelitaka jeshi la polisi kuchukukuliwa hatua za kinidhamu ili kuweza kukomesha tabia hizo.

 

Comments are closed.