KITUO CHA KULELEA WATOTO YATIMA NEW HOPE FAMILY CHAZINDUA KIKOMBE CHA AMANI NA UPENDO KUELEKEA UCHAGUZI MKUU

KITUO CHA KULELEA WATOTO YATIMA NEW HOPE FAMILY CHAZINDUA KIKOMBE CHA AMANI NA UPENDO KUELEKEA UCHAGUZI MKUU

Like
436
0
Wednesday, 11 March 2015
Local News

KATIKA kudumisha Amani na Upendo kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Madiwani,Wabunge na Rais pamoja na Upigaji Kura za Maoni kwa Katiba mpya, Kituo cha Kulea Watoto Yatima cha New Hope Family kimezindua Kikombe cha Amani na Upendo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa Kituo hicho OMARI  KOMBE amesema, Kikombe hicho kitazunguka maeneo mbalimbali ya nchi ili kuhamasisha Watanzania kudumisha amani kama ilivyodumishwa na aliyekuwa Baba wa Taifa Mwalim JULIUS NYERERE

Pia KOMBE amelaani Vitendo vinavyofanywa na baadhi ya watu wanaofanya Mauaji dhidi ya Watu wenye Ulemavu wa Ngozi na Vikongwe kwani kufanya hivyo  ni uvunjifu wa Amani hivyo amevitaka Vyombo vya Sheria kutoa adhabu dhidi ya watuhumiwa wanaobainika.

Comments are closed.