KITUO CHA MICHEZO CHA JMK KUZINDULIWA RASMI OKTOBA 17 NA RAIS KIKWETE

KITUO CHA MICHEZO CHA JMK KUZINDULIWA RASMI OKTOBA 17 NA RAIS KIKWETE

Like
251
0
Thursday, 01 October 2015
Local News

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete Oktoba 17, mwaka huu atazindua rasmi Kituo cha Michezo cha Kisasa cha Jakaya M. Kikwete Youth Park (JMK Park), Kidongo Chekundu, Dar es Salaam, kikiwa ni kituo cha kwanza cha aina yake nchini chenye kulenga miongoni mwa mambo mengi kuanza kulea wanamichezo tokea wakiwa wadogo.

 

Rais Kikwete alikubali kuzindua Kituo hicho wakati wa mazungumzo kati yake na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Umeme ya Symbion Power, Bwana Paul Hinks kwenye Hoteli ya JW Marriot Essex House, mjini New York, Marekani ambako Rais alikuwa anafanya ziara rasmi ya kikazi.

 

Bwana Hinks amemweleza Rais Kikwete kuwa ujenzi wa Kituo hicho sasa umekamilika tayari kwa uzinduzi na hivyo kuongeza thamani kubwa kwenye eneo ambalo miaka ya nyuma lilikuwa gereji ya kutengenezea magari.

Comments are closed.