KLINIKI YA LOTUS KWA  KUSHIRIKIANA NA HOSPITALI YA MUHIMBILI ZAANZISHA KAMPENI YA KUELIMISHA UMA JUU YA UGONJWA WA USONJI

KLINIKI YA LOTUS KWA KUSHIRIKIANA NA HOSPITALI YA MUHIMBILI ZAANZISHA KAMPENI YA KUELIMISHA UMA JUU YA UGONJWA WA USONJI

Like
311
0
Monday, 01 June 2015
Local News

KLINIKI ya Lotus kwa kushirikiana na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, zimeanzisha kampeni mpya inayolenga kuelimisha uma kuhusu ugonjwa wa usonji ambao watanzania wengi hawana ufahamu wa kutosha juu ya ugonjwa huo.

Akizugumza wakati wa uzinduzi huo Jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Chama cha Kuhudumia watu wenye Usonji Tanzania dokta STELLA RWEZAULA kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ameahidi kuwa mstari wa mbele kuwezesha kampeni hiyo ili kuwaelimisha watanzania kuhusu ugonjwa huo.

Ugomjwa huu sasa unatishia familia nyingi kwani dalili zake huanza utotoni na zinaweza kuendelea hadi ukubwani kwa kuhusisha shida katika kuwasiliana na kwamba tabia zao ni kurudia rudia mambo anayofanya mara kwa mara.

Comments are closed.