Mmoja wa nyota wa mpira wa vikapu duniani Kobe Bryant, amecheza mechi yake ya mwisho ya kulipwa nchini Marekani.
Mchezo huo utafikisha kikomo uchezaji wake wa zaidi ya miongo miwili ambapo Bryant amekuwa wa tatu kwa kuandikisha alama nyingi zaidi katika historia ya mchezo huo.
Alishinda mataji matano ya NBA akiwa na LA Lakers ambao amewachezea muda wote huo.
Lakini mwandishi mmoja wa BBC anasema Bryant hajaenziwa kwa njia sawa na mashabiki.
Wakati mwingine alikuwa hachezaji vyema na mara kwa mara alikorofishana na machezaji mwenzake, Shaquille O’Neal.
Mwaka 2003 alituhumiwa kumbaka mwanamke mmoja lakini baadaye wakaafikiana na kumaliza kesi nje ya mahakama.
Bryant, ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 37 alianza kucheza katika ligi ya NBA moja kwa moja baada ya kumaliza shule ya upili akiwa na umri wa miaka 17.
Aliweka rekodi ya kuwa mchezaji mchanga zaidi kujiunga na NBA, akicheza dhidi ya Dallas akiwa na umri wa miaka 18, miezi miwili na siku 11.