KOBE BRYANT ACHEZA MECHI YAKE YA MWISHO

KOBE BRYANT ACHEZA MECHI YAKE YA MWISHO

Like
272
0
Thursday, 14 April 2016
Slider

Mmoja wa nyota wa mpira wa vikapu duniani Kobe Bryant, amecheza mechi yake ya mwisho ya kulipwa nchini Marekani.

Mchezo huo utafikisha kikomo uchezaji wake wa zaidi ya miongo miwili ambapo Bryant amekuwa wa tatu kwa kuandikisha alama nyingi zaidi katika historia ya mchezo huo.

Alishinda mataji matano ya NBA akiwa na LA Lakers ambao amewachezea muda wote huo.

LOS ANGELES, CA - NOVEMBER 16:  Kobe Bryant #24 of the Los Angeles Lakers takes a shot against the Golden State Warriors on November 16, 2014 at Staples Center in Los Angeles, California. NOTE TO USER: User expressly acknowledges and agrees that, by downloading and or using this Photograph, user is consenting to the terms and conditions of the Getty Images License Agreement. Mandatory Copyright Notice: Copyright 2014 NBAE (Photo by Andrew D. Bernstein/NBAE via Getty Images)

Tiketi za mechi hiyo yake ya mwisho, dhidi ya Utah Jazz uwanja wa Staples Center mjini Los Angeles, California zimekuwa zikiuzwa hadi dola 30,000 za Kimarekani.

Lakini mwandishi mmoja wa BBC anasema Bryant hajaenziwa kwa njia sawa na mashabiki.

Wakati mwingine alikuwa hachezaji vyema na mara kwa mara alikorofishana na machezaji mwenzake, Shaquille O’Neal.

Mwaka 2003 alituhumiwa kumbaka mwanamke mmoja lakini baadaye wakaafikiana na kumaliza kesi nje ya mahakama.

Bryant, ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 37 alianza kucheza katika ligi ya NBA moja kwa moja baada ya kumaliza shule ya upili akiwa na umri wa miaka 17.

Aliweka rekodi ya kuwa mchezaji mchanga zaidi kujiunga na NBA, akicheza dhidi ya Dallas akiwa na umri wa miaka 18, miezi miwili na siku 11.

Comments are closed.