KOCHA WA ZAMANI WA YANGA, MICHO AJIUNGA NA AL HILAL YA SUDANI

KOCHA WA ZAMANI WA YANGA, MICHO AJIUNGA NA AL HILAL YA SUDANI

Like
509
0
Monday, 09 March 2015
Slider

Kocha wa zamani wa Yanga, Micho ajiunga na klabu ya Al Hilal ya Sudani na kuitosa timu ya Taifa ya Uganda

Timu hiyo ya sudani imemtangaza mserbia Milutin ‘Micho’ Sredojevic kama kocha mkuu w timu hiyo baada ya kikao cha bodi siku ya jumamosi

Al Hilal imemaliza mkataba wake na kocha aliekuwa akikinoa kikosi hicho Patrick Osimes mwezi uliopita.

“Bodi imekutana jumamosi katika makao makuu ya klabu huko Omdurman na kufikia maamuzi mengi ikiwemo kumchagua Micho kuwa kocha mkuu” ilitangaza klabu hiyo

Micho mwenye umri wa miaka 45 alianza rasmi fani hiyo ya ualimu mwaka 1994 na alishawahi kufanyakazi na klabu ya Al Hilal mnamo mwaka 2010 hadi 2011 kabla hajaenda kuwa kocha mkuu wa timu za taifa Rwanda na Uganda

Comments are closed.