Koffi Annan kuzikwa Ghana, Alhamisi

Koffi Annan kuzikwa Ghana, Alhamisi

Like
491
0
Tuesday, 11 September 2018
Global News

Mwili wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan, umewasili katika nchi Ghana.

Mwili wake umewasili katika Uwanja wa Ndege wa  Kimataifa wa Kotoka uliopo mjini Accra, ukisindikizwa na familia yake na maafisa wengine wa Umoja wa Mataifa.

Anatarajiwa kuzikwa kitaifa siku ya Alhamisi ya Taehe 13, September 2018

Kulikuwa na hali ya maombolezowakati mwili wake ukiwasili uwanjani hapo na kupokelewa na Rais wa Ghana Akufo Addo na viongozi wa kimila na kwa heshima ya kijeshi.

Mwili wake umehifadhiwa katika Ukumbi wa Kimataifa wa mikutano wa Ghana, wakati ukisubiri kuzikwa.

Kofi Annan alikuwa ni Katibu mkuu wa kwanza wa Umoja wa Mataifa, kutoka katika eneo la kusini mwa jangwa la Sahara na kuleta mafanikio sio tu katika bara la Afrika, lakini pia dunia nzima.

Aliwahamasisha vijana wengi nchini mwake na waliheshimu kile alichosimamia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *