KONGAMANO LA KIMATAIFA KUFANYIKA LEO

KONGAMANO LA KIMATAIFA KUFANYIKA LEO

Like
275
0
Friday, 21 November 2014
Local News

 

KONGAMANO la Kimataifa la Masuala ya Uongozi linafanyika leo jijini Dar es salaam kwa lengo la kujifunza Misingi ya Uongozi bora, Barani Afrika.

Akizungumza na waandishi wa habari Mwenyekiti wa Kongamano hilo MBUTHO CHIBWAYE amesema kuwa kongamano hilo litasaidia kuleta mabadiliko na maendeleo chanya katika nchi za Afrika.

Mbutho amebainisha kuwa Kongamano litachangia kutatua migogoro inayo sababisha machafuko ya kisiasa na kijamii.

Aidha ametoa wito kwa Watanzania wote nchini kujitokeza na kushiriki Kongamano hilo.

Comments are closed.