KONGO: DENIS SASSOU AATANGAZWA KUWA MSHINDI WA UCHAGUZI

KONGO: DENIS SASSOU AATANGAZWA KUWA MSHINDI WA UCHAGUZI

Like
256
0
Wednesday, 23 March 2016
Global News

KIONGOZI wa muda mrefu nchini Kongo, Denis Sassou Nguesso, ametangazwa na Tume ya Uchaguzi nchini humo kushinda tena urais, na hivyo kumpa nafasi ya kuendeleza utawala wake wa zaidi ya miongo mitatu sasa.

 

Huku matokeo ya mji mkuu wa kiuchumi na ngome ya upinzani, Pointe-Noire, yakiwa hayajajumuishwa, mkuu wa tume ya uchaguzi, Henri Bouka, amesema Nguesso tayari ana asilimia 67 ya kura.

 

Mwanajeshi huyo wa zamani wa kikosi cha miamvuli kwenye jeshi la Ufaransa na mwenye umri wa miaka 72, amekuwa madarakani kwa miaka 32 sasa.

Comments are closed.