TAIFA la Korea Kaskazini limerusha makombora mawili ya masafa marefu katika bahari ya mashariki ya pwani yake, siku chache baada ya kiongozi wake Kim Jong-un kuagiza majaribio ya mabomu zaidi ya kinyuklia na silaha nyingine.
Marekani imejibu kwa kutoa wito kwa Pyongyang kutozua wasiwasi katika eneo hilo ambao umekua juu tangu Korea Kaskazini ifanye jaribio la nne la mabomu yake ya kinyuklia mnamo mwezi Januari.
Korea Kusini imeelezea jaribio hilo la hivi karibuni kama tishio kubwa la usalama na udhibiti wa eneo hilo.