KOREA KASKAZINI YASHINDWA KURUSHA KOMBORA

KOREA KASKAZINI YASHINDWA KURUSHA KOMBORA

Like
278
0
Friday, 15 April 2016
Local News

KOREA Kaskazini imefanya jaribio la kufyatua kombora katika pwani yake ya mashariki, lakini dalili zinaonesha jaribio hilo halikufanikiwa, kwa mujibu wa maafisa wa Marekani na Korea Kusini.

Bado haijabainika roketi iliyotumiwa ilikuwa ya aina gani lakini inadhaniwa majaribio hayo yalikuwa ya kombora la masafa ya wastani kwa jina “Musudan” ambalo taifa hilo lilikuwa halijalifanyia majaribio.

Shughuli hiyo ilikuwa ikifanyika siku ambayo ni ya kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwa mwanzilishi wa taifa la Korea Kaskazini Kim Il-sung.

Comments are closed.