KOREA KUPUNGUZA HALI YA WASIWASI MPAKANI

KOREA KUPUNGUZA HALI YA WASIWASI MPAKANI

Like
202
0
Tuesday, 25 August 2015
Global News

NCHI za Korea kaskazini na Kusini zimefikia makubaliano ya kupunguza hali ya wasiwasi iliyopo mpakani mwa nchi hizo mbili.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya mazungumzo ya muda mrefu ambapo nchi zote mbili ziliweka vikosi vyake vya ulinzi kama tahadhari baada ya mapigano ya muda mfupi yaliyotokea wiki iliyopita.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na pande hizo mbili, Korea kusini imekubali kuacha kueneza habari zenye propaganda zinazochochea pande hizo, huku Korea kaskazini ikielezea masikitiko yake juu ya tukio la hivi karibuni la utegaji bomu lililojeruhi wanajeshi wawili wa Korea kusini.

Comments are closed.