Korea Kusini na Kaskazini kufanya mkutano wiki ijayo

Korea Kusini na Kaskazini kufanya mkutano wiki ijayo

Like
481
0
Saturday, 24 March 2018
Global News


Korea Kusini na Korea Kaskazini ambazo zimekuwa mahasimu kwa muda mrefu, zimekubaliana kufanya mkutano wa ngazi ya juu wiki ijayo ili kufanya maandalizi ya mkutano wa Aprili kati ya Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un na Rais wa Korea Kusini Moon Jae-in. Korea Kusini imesema mkutano huo unalenga kuimarisha uhusiano na kusuluhisha mkwamo kuhusu mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini. Waziri wa Muungano Cho Myoung-gyon ataongoza ujumbe wa Korea kusini katika mkutano huo ambao umepangwa kufanyika tarehe 29 Machi katika mji wa mpakani wa Panmunjom. Ujumbe wa Korea Kaskazini utaongozwa na mwenyekiti wa shirika linaloshughulikia masuala yanayohusu nchi hizo mbili Ri Son Gwon. Maafisa watajadili tarehe ya mkutano wa marais wa nchi hizo, miongoni mwa ajenda nyinginezo maalum. Viongozi wa Korea hizo mbili wamefanya mazungumzo mara mbili pekee tangu vita vya Korea vilivyodumu kati ya mwaka 1950-1953.

Comments are closed.