KOREA KUSINI NA MAREKANI ZATANGAZA KUANZA MAZOEZI YA KIJESHI

KOREA KUSINI NA MAREKANI ZATANGAZA KUANZA MAZOEZI YA KIJESHI

Like
322
0
Tuesday, 24 February 2015
Global News

KOREA ya Kusini na Marekani zimetangaza hivi leo kwamba zitaanza mazoezi yao ya kila mwaka ya kijeshi tarehe 2 mwezi ujao, hatua inayotazamiwa kuongeza mzozo na Korea Kaskazini.Serikali ya Korea Kaskazini ilikuwa imeahidi kusitisha majaribio yake ya silaha za nyuklia, endapo mazoezi hayo yangefutwa mwaka huu, lakini Marekani ililikataa pendekezo hilo ikiliita “kitisho” cha kufanya jaribio la nne la nyuklia.

Mazoezi hayo ya pamoja ndicho kiini cha mzozo wa mara kwa mara kwenye Rasi ya Korea, ambayo Korea Kaskazini huyachukulia kama kitendo cha uchokozi, ingawa Marekani na Korea Kusini zinadai kuwa ni mazoezi ya kujilinda.

Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un, amelitaka jeshi la nchi yake kuwa tayari kujibu “uchokozi wowote wa adui.”

 

Comments are closed.