KRIKETI: TANZANIA KUCHUANA NA UGANDA KWENYE MICHUANO YA UFUNGUZI AFRIKA KUSINI

KRIKETI: TANZANIA KUCHUANA NA UGANDA KWENYE MICHUANO YA UFUNGUZI AFRIKA KUSINI

Like
292
0
Thursday, 26 March 2015
Slider

Tanzania kuchuana na Uganda kwenye mechi ya ufunguzi ya michuano ya Afrika Ligi Daraja la 1 inayotarajiwa kufanyika katika mji wa Benoni huko nchini Afrika kusini

Timu teule ya mchezo huo wa Kriketi tayari imeondoka nchini kuelekea Afrika ya kusini kujiandaa na mchezo huo

Kikosi hicho cha Tanzania kinaongozwa na nahodha Hamisi Abdallah mwenye uzoefu wa kushiriki michuano ya kimataifa ya mchezo wa kriketi akiichezea Tanzania kwa nafasi hiyo zaidi ya miaka 10 huku akiwa na rekodi ya kucheza kriketi nchini Uingereza katika klabu ya Watford Town.

Nahodha huyo amekizungumzioa kikosi cha Uganda kuwa sio timu ngeni na wanaichukulia mechi yao kwa umuhimu mkubwa.

Nchi nyingine zinazotarajiwa kushiriki kwenye michuano hiyo ni pamoja na Kenya, Namibia, Botswana na Ghana.

Comments are closed.