KACHERO WA ISRAEL AKAMATWA NA KUNDI LA HEZBOLLAH

KACHERO WA ISRAEL AKAMATWA NA KUNDI LA HEZBOLLAH

Like
222
0
Friday, 16 January 2015
Global News

KIONGOZI wa kundi la wapiganaji wa Kilebanoni la Hezbollah amethibitisha taarifa zinazodai kuwepo mmoja wa viongozi wa juu ndani ya kundi hilo anatuhumiwa kutumwa na Israel kuwapepeleza.

Shekh Sheikh Hassan Nasrallah amesema kiongozi huyo anayetuhumiwa tayari anashikiliwa na kundi hilo tangu abainike miezi mitano wakati akifanya kazi kwenye idara ya usalama ya kundi hilo la Hezbollah.

Kauli ya Shekh Nasrallah imekuja siku chache baada ya kutolewa taarifa kupitia vyombo vya habari vya Lebanon zinazodai kuwepoa kwa ofisa wa ngazi za juu wa Israel miongoni mwa wapiganaji haoa ambaye yupo kwa kazi maalum.

 

Comments are closed.