WATANZANIA leo wanakumbuka kuzaliwa kwa aliyekuwa Mwasisi wa Taifa hilo na Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere ambaye alizaliwa tarehe 13 mwezi wa nne mwaka 1922 katika familia ya kichifu.
Hayati Nyerere ambaye alikuwa rais wa kwanza wa Tanzania, alizaliwa, kulelewa na kukua kama watoto wengine wa vijijini akiwasaidia wazazi wake kwa shughuli za kilimo na kuchunga mifugo, moja ya shughuli muhimu za Kiuchumi kwa jamii ya Wazanaki kutoka kijiji cha Butiama, Wilaya ya Musoma, Mkoani Mara.
Akizungumzia kumbukumbu hiyo mjumbe wa Tume ya Uchaguzi nchini-NEC-Profesa AMON CHALIGHA amesema kuwa hayati Mwalimu Nyerere alikuwa ni kiongozi mwadilifu na anapaswa kuwa mfano wa kuigwa kwa viongozi wa sasa.