KUMI WAUAWA MALI

KUMI WAUAWA MALI

Like
190
0
Monday, 10 August 2015
Global News

JESHI nchini Mali limesema zaidi ya watu kumi wameuawa katika shambulio moja kwenye mji wa Gaberi kaskazini nchini humo.

Shambulizi hilo limekuja siku moja baada ya watu kumi na watatu wakiwemo washambuliaji wanne kuuawa ambapo washukiwa wa tukio hilo Wanajeshi wa Kiislam walishambuliana na jeshi la serikali walipowazingira kwenye hotel moja katikati mwa mji wa Sevare.

Msemaji wa jeshi la Mali alikaririwa akisema ni mapema mno kujua kama mashambulizi hayo mawili yalikua na uhusiano ama la.

Comments are closed.