KUNA UWEZEKANO WA KURUDISHA CHENJI KWA MASHABIKI AFRIKA?

KUNA UWEZEKANO WA KURUDISHA CHENJI KWA MASHABIKI AFRIKA?

Like
367
0
Wednesday, 22 October 2014
Slider

Wachezaji wa Sunderland wameamua kuwarudishia Mashabiki wao gharama walizotumia kuutizama mchezo ambao mwisho wa siku walipokea kichapo cha bao 8-0 kutoka kwa Southampton.

Hicho kilikuwa kisago kikubwa kabisa kwa Sunderland katika miaka 32.

Mashabiki wana nafasi ya kudai pesa yao mpaka kufikia tarehe 5 ya Novemba mwaka huu.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake, nahodha John O’Shea amesema, “Tunashinda na kushindwa kama timu, wachezaji, uongozi na mashabiki lakini tungependa kuwatambua na kuwashukuru mashabiki waliosafiri umbali mrefu kuja kutuunga mkono na pamoja na yote yaliyotokea walibaki nasi mpka filimbi ya mwisho”

Mashabiki wameombwa kurejesha tiketi au hata kuzituma kwa njia ya posta wakiambatanisha na majina na anwani zao kamili.

Mashabiki ambao hawatadai pesa yao basi pesa hiyo waliyoitumia katika manunuzi ya Tiketi zitapelekwa katika kituo cha kutunzia watoto.


 

Comments are closed.