MAHAKAMA ya juu zaidi nchini Brazil imekataa ombi la serikali la kutaka kutupiliwa mbali kura ya bunge kuamua ikiwa rais Dilma Rousseff ataondolewa madarakani.
Mahakama imekataa kufuta amri ya kupiga kura iliyoamuliwa na spika wa bunge la chini, ambayo itaamua siku ya Jumapili ikiwa Rousseff ataondolewa madarakani au la.
Wafuasi wa rais huyo, walikuwa wamedai kuwa zoezi hilo litavurugwa kwa sababu wabunge kutoka majimbo yanayompinga Rousseff huenda wakapiga kura kwanza. Bi Rousseff amelaumiwa kwa kuvuruga bajeti kabla ya uchaguzi wa mwaka 2014 madai ambayo anayapinga.