KURA YA MAONI KUAMUA HATMA YA MGOGORO WA KIUCHUMI UGIRIKI

KURA YA MAONI KUAMUA HATMA YA MGOGORO WA KIUCHUMI UGIRIKI

Like
216
0
Thursday, 02 July 2015
Global News

WAZIRI MKUU wa Ugiriki Alexis Tsipras amesisitiza kura ya maoni aliyoitisha  siku ya Jumapili wiki hii itaamua hatma ya mgogoro wa kiuchumi unaoikumba nchi yake.

Mawaziri wa fedha wa kanda inayotumia sarafu ya euro waliokutana hapo jana wamesema hawatafanya mkutano mwingine wa kuzingatia maombi yoyote mapya ya kuipa nchi hiyo mkopo wa uokozi hadi kura hiyo ya maoni itakapofanyika.

Tsipras amesema kura ya kupinga masharti magumu ya wakopeshaji wa Ugiriki haimaniishi nchi hiyo inajiondoa kutoka Umoja wa Ulaya bali ni kura ya kutaka kurejea kwa msingi wa maadili ya umoja huo.

 

Comments are closed.