KURA ZAANZA KUHESABIWA BURUNDI

KURA ZAANZA KUHESABIWA BURUNDI

Like
157
0
Wednesday, 22 July 2015
Global News

SHUGHULI ya kuhesabu Kura imeanza nchini Burundi kufuatia uchaguzi wa urais ambao umeshutumiwa na wengi nchini humo na hata kimataifa.

Rais Pierre Nkurunzinza anatarajiwa kupata ushindi mkubwa kwa muhula wa tatu huku upinzani ukisusia kabisa kura hiyo.

Huku hayo yakijiri Marekani na Uingereza wamekashifu kura hiyo wakisema kuwa haikuwa ya huru na haki.

Marekani kwa upande wake imependekeza kugawana madaraka huku ikitishia kuchukua hatua dhidi ya Burundi iwapo muafaka hautapatikana.

Comments are closed.