KURA ZAHESABIWA AFRIKA YA KATI

KURA ZAHESABIWA AFRIKA YA KATI

Like
211
0
Monday, 15 February 2016
Global News

MAAFISA wa uchaguzi wanaendelea kuhesabu kura baada ya Jamhuri ya Afrika ya Kati kuandaa jana awamu ya pili iliyocheleweshwa ya uchaguzi wa rais na wabunge, ikiwa na matumaini ya kupatikana amani baada ya kutokea machafuko makubwa ya kidini kuwahi kushuhudiwa nchini humo tangu uhuru mwaka wa 1960.

Upigaji kura ulifanywa chini ya ulinzi mkali huku maelfu ya wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa wakiwekwa kote nchini humo, lakini uchaguzi huo ulikamilika kwa amani.

Matokeo ya mwanzo yanatarajiwa kutangazwa baada ya siku kadhaa.

Comments are closed.