KUTOKUJUA SHERIA KWA WAZEE WA MABARAZA YA KATA KUNACHANGIA MIGOGORO KATIKA JAMII

KUTOKUJUA SHERIA KWA WAZEE WA MABARAZA YA KATA KUNACHANGIA MIGOGORO KATIKA JAMII

Like
394
0
Tuesday, 11 November 2014
Local News

KUTOKUJUA masuala ya Sheria kwa Wazee wa Mabaraza ya Kata kunachangia migogoro katika jamii na kusababisha kuwa na mlundikano wa Kesi Mahakamani jambo ambalo linapaswa kumalizwa katika Mabaraza hayo.

 

Hayo yamebainishwa na Ofisa Utumishi wa Halmashauri ya Rungwe CHRISTOPHER NYAMBAZA alipokuwa akifunga mafunzo ya Wiki Moja ya Wasaidizi wa Kisheria kwa Niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo yaliyotolewa na Shirika la la House of Peace.

 

NYAMBAZA amebainisha kuwa Halmashauri itaangalia uwezekano wa kuwaingiza kwenye Mabaraza ya Kata ya Ushauri wa Vijana waliopitia Mafunzo ya usaidizi wa Kisheria ili kupunguza Migogoro isiyokuwa na sababu kutokana na Madai yao kupindishwa kwa kutokuwa na ufahamu wa kisheria kwa Wazee na Mabaraza.

Comments are closed.