LAMORDE AKANUSHA UFISADI NIGERIA

LAMORDE AKANUSHA UFISADI NIGERIA

Like
254
0
Thursday, 27 August 2015
Global News

MKURUGENZI mkuu wa shirika la kupambana na ufisadi nchini Nigeria-EFCC– Ibrahim Lamorde amekanusha madai kuwa zaidi ya dola bilioni tano zimetoweka kutoka kwa hazina ya shirika hilo.

Lamorde amesema kuwa hata fedha zilizokusanywa na –EFCC- zikijumuishwa na ufadhili wote unaotolewa na shirika hilo, haziwezi kufika dola bilioni tano kwa pamoja.

Aidha ameliambia shirika la utangazaji la BBC kuwa madai hayo hayana msingi na yananuia kumharibia sifa, kwa sababu EFCC kwa sasa bado inamchunguza mtu aliyetoa madai hayo.

Comments are closed.