LEO NI SIKU YA KIMATAIFA YA KUPINGA UKEKETAJI

LEO NI SIKU YA KIMATAIFA YA KUPINGA UKEKETAJI

Like
335
0
Friday, 06 February 2015
Global News

LEO ni siku ya kimataifa ya kupinga ukeketaji. Umoja wa Mataifa ulianzisha siku hiyo kuhimiza jamii zinazowakeketa wanawake na wasichana kuacha mila hiyo ambayo inaleta athari kubwa za kiafya na kisaikolojia.

Takwimu za Umoja wa Mataifa zinaonyesha kwamba duniani kote wapo wasichana na wanawake milioni 140 waliokeketwa.

Umoja wa Mataifa unaonya kuwa idadi ya wataalamu wa afya wanaowakeketa wasichana inaongezeka, suala linalorudisha nyuma juhudi za kuitokomeza mila hiyo.

 

 

Comments are closed.