LEO NI SIKU YA KUMBUKUMBU YA KUZALIWA KWA MWL. JK NYERERE

LEO NI SIKU YA KUMBUKUMBU YA KUZALIWA KWA MWL. JK NYERERE

Like
418
0
Monday, 13 April 2015
Local News

WATANZANIA leo wanakumbuka kuzaliwa kwa aliyekuwa Mwasisi wa Taifa hilo na Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere ambaye alizaliwa tarehe 13 mwezi wa nne mwaka 1922 katika familia ya kichifu.

Hayati Nyerere ambaye alikuwa rais wa kwanza wa Tanzania, alizaliwa, kulelewa na kukua kama watoto wengine wa vijijini akiwasaidia wazazi wake kwa shughuli za kilimo na kuchunga mifugo, moja ya shughuli muhimu za Kiuchumi kwa jamii ya Wazanaki kutoka kijiji cha Butiama, Wilaya ya Musoma, Mkoani Mara.

Kumekuwepo na maoni miongoni mwa watu na viongozi Nchini kuhusu siku hasa ya kumbukumbu ya Kitaifa ya Mwalimu Nyerere kwamba ifanyike siku yake ya kuzaliwa au siku yake ya kufariki dunia.

 

Comments are closed.