LEWIS HAMILTON AONGEZA MKATABA KUITUMIKIA MERCEDES

LEWIS HAMILTON AONGEZA MKATABA KUITUMIKIA MERCEDES

Like
301
0
Tuesday, 31 March 2015
Slider

Bingwa wa dunia wa mbio za magari Lewis Hamilton anatarajiwa kusaini mkataba mpya wiki hii utakaomwingizia zaidi ya pound milioni 27 kwa mwaka.

Hamilton mwenye umri wa miaka 30 raia wa Uingereza amekuwa kwenye mazungumzo na viongozi wa kampuni ya magari ya Mercedes ambapo dili hilo nono kwa dereva huyu lipo kwenye hatua za mwisho kumaliziwa na wanasheria.

Hamilton amesema mchakato wa kusaini mkataba huo utamalizika wiki hii wala hakuna sababu itakayokwamisha kwani hakuna makubaliano yaliyoachwa hivyo mchakato huo umekamilika kwa asilimia 99%

 

Dereva huyu wa formular one alijiunga na kampuni ya Mercedes mwaka 2013 baada ya miaka sita ya kuitumikia kampuni ya McLaren

Comments are closed.