Lewis Hamilton kinara majaribio ya Australian GP, awafunika Ferrari na Red Bull

Lewis Hamilton kinara majaribio ya Australian GP, awafunika Ferrari na Red Bull

Like
361
0
Friday, 23 March 2018
Sports

Lewis Hamilton

Dereva wa kampuni ya Mercedes, Lewis Hamilton ameibuka kinara kwenye majaribio ya magari kabla ya kuanza kwa mashindano ya Australian GP yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi leo Machi 23 siku ya Ijumaa.

Hamilton ameibuka kinara mara mbili kwenye mashindano hayo maarufu kwa jina la Formula One (F1) msimu huu wa mwaka 2018 na kuwazidi washindani wake wakubwa Ferrari na Red Bull.

Licha ya kuongoza kwa magari hayo ya kampuni ya Mercedes yalipata ushindani mkubwa kwenye mbio hizo za majaribio kabla ya mashindano kutoka kwa Red Bull na Ferrari.

Bingwa huyo wa dunia wa mashindano ya Formula One, Lewis Hamilton amemaliza wa kwanza kwenye mbio hizo za majaribio akimzidi Max Verstappen wa Red Bull aliyeshika nafasi ya pili kwa sekunde 0.7.

Comments are closed.