LIBERIA: GWIJI LA SOKA, GEORGE WEAH ATANGAZA KUWANIA URAIS KWA MARA YA PILI

LIBERIA: GWIJI LA SOKA, GEORGE WEAH ATANGAZA KUWANIA URAIS KWA MARA YA PILI

Like
272
0
Friday, 29 April 2016
Local News

GWIJI wa Soka la Kimataifa wa  Liberia George Weah ametangaza rasmi kuwa atawania nafasi ya urais wa nchi hiyo kwa mara ya pili.

Weah, ambaye aliwahi kuchezea klabu za PSG, AC Milan, Chelsea,  na Monaco amebainisha kwamba amekuwa na malengo ya kuliletea Taifa hilo mabadiliko, tangu alipoanza kujihusisha na masuala ya kisiasa mara tu baada ya kurejea Liberia mwaka 2003.

Rais wa Sasa Johnson Sirleaf anamaliza awamu yake ya pili na ya mwisho katika utawala wake mwaka  2017  ambapo kwa mujibu wa Katiba ya nchi hiyo hataweza tena kuwania nafasi hiyo.

Comments are closed.