LIBYA: MAKUNDI HASIMU  YAMETAKIWA KUTOKWAMISHA MIPANGO YA KUGAWANA MADARAKA

LIBYA: MAKUNDI HASIMU YAMETAKIWA KUTOKWAMISHA MIPANGO YA KUGAWANA MADARAKA

Like
327
0
Friday, 06 November 2015
Global News

MJUMBE  wa  Umoja  wa  Mataifa  nchini  Libya  ambaye anaondoka  ameyataka  makundi  hasimu  nchini  humo  kusitisha  juhudi  zao  za  kuzuwia  mpango  wa kugawana  madaraka unaolenga  katika  kumaliza  mzozo wa  kisiasa  nchini  mwao.

Bernardino  Leon, ambaye  nafasi  yake  inatarajiwa kuchukuliwa  hivi  karibuni  na  mwanadiplomasia  wa  siku nyingi  wa  Ujerumani,  Martin Kobler, pia  amejitetea  dhidi ya  maelezo  kwamba  kuna  mvutano  wa  kimaslahi kwake  kukubali  kazi  katika  Umoja  wa  Falme  za Kiarabu  kuwapa  mafunzo  wanadiplomasia  kutoka  moja kati  ya  mataifa  ya  Kiarabu ambayo  inahusika  sana  na mzozo  wa  Libya.

 

Comments are closed.