LIBYA YAOMBA KUONDOLEWA VIKWAZO VYA SILAHA KULINDA USALAMA WAKE

LIBYA YAOMBA KUONDOLEWA VIKWAZO VYA SILAHA KULINDA USALAMA WAKE

Like
157
0
Thursday, 19 February 2015
Global News

SERIKALI ya Libya inayotambuliwa Kimataifa imeliomba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuiondolea nchi hiyo vikwazo vya silaha ili kukabiliana na kuzorota kwa hali ya Usalama nchini humo.

Akihutubia Kikao cha dharura cha Baraza hilo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Libya,MOHAMMED AL-DAIRI amesema hatua hiyo itaisaidia Serikali ya Libya kujenga jeshi lake, ili kuwatokomeza Islamic State na makundi mengine ya Wapiganaji.

Waziri huyo wa Mambo ya nje wa Libya ameungwa mkono na Waziri wa Mambo ya nje wa Misri SAMEH SHOUKRY, ambaye amesema jumuia ya kimataifa inatakiwa kuisaidia serikali ya Libya ili kuonyesha mamlaka yake nchini humo.

Comments are closed.