LIPUMBA ATANGAZA NIA YA KUPEPERUSHA BENDERA YA UKAWA

LIPUMBA ATANGAZA NIA YA KUPEPERUSHA BENDERA YA UKAWA

Like
291
0
Monday, 01 June 2015
Local News

 MWENYEKITI wa Chama cha wananchi –CUF-Profesa IBRAHIM LIPUMBA huenda akaingia kwa mara ya tano katika mbio za kuwania nafasi ya uraisi endapo Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA utampitisha kugombea nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Lipumba ametangaza nia ya kugombea nafasi hiyo ya juu ya kisiasa nchini juzi mjini Tabora wakati wa mikutano yake ya hadhara ya kuhamasisha wananchi kujitokeza kujiandikisha kupiga kura kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu

Profesa Lipumba anakuwa mwanasiasa wa tatu kutoka vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi –Ukawa– kutangaza nia hiyo baada ya mwenyekiti wa NLD Emmanuel Makaidi na dokta George Kahangwa wa NCCR-Mageuzi kujitokeza kutaka kuongoza Serikali ya Awamu ya Tano

Comments are closed.