LIVERPOOL KUMCHUNGUZA RAHEEM STERLING

LIVERPOOL KUMCHUNGUZA RAHEEM STERLING

Like
255
0
Tuesday, 14 April 2015
Slider

Raheem Sterling arejesha matumaini kwa klabu ya soka ya Liverpool kuingia kwenye top four kwenye ligi ya Uingereza lakini pia kujihakikishia nafasi kwenye msimu ujao wa ligi ya mabingwa baada ya kuichabanga 2-0 klabu ya Newcastle United katika uwanja wa Anfield hapo jana.

Kikosi cha Newcastle United kilimpoteza nahodha wa timu hiyo Moussa Sissoko alietolewa nje ya mchezo kwa kadi kwenye dakika ya saba

Sterling mwenye umri  wa miaka 20 ameingia kwenye wakati mgumu kufuatia kunaswa kwa video inayomuonesha akivuta  shisha siku ya jumapili hivyo basi kwa sasa ataingia kwenye uchunguzi maalum kutoka kwenye klabu yake ya Liverpool

Video hiyo inamuonyesha mchezaji huyo akivuta shisha na marafiki zake na baadae anaonekana hajitambui kabisa kutokana na kilevi kilichomo ndani yake ambapo inasadikika kuwa video hiyo ilichukuliwa siku moja kabla ya mechi

Comments are closed.