LIVERPOOL YAKUBALI KUMSAJILI BENTEKE

LIVERPOOL YAKUBALI KUMSAJILI BENTEKE

Like
263
0
Monday, 20 July 2015
Slider

Liverpool imekubali kumsajili mshambuliaji Christian Benteke kutoka kwa wapinzani wao kwenye Premier League klabu ya Aston Villa kwa kitita cha pound milioni 32.5.

Mchezaji huyo wa kimataifa kutoka Ubelgiji  mwenye miaka 24 kwa sasa anafanyiwa vipimo na daktari wa klabu ya Liverpool.

Benteke aliwasili Villa akitokea Genk kwa pound milioni 7 mwaka 2012 akiwa na rekodi ya magoli 49 katika michezo 101 na klabu ya Birmingham.

Liverpool inamchukua nyota huyu akiwa amebakiza miaka miwili katika mkataba wake na Villa

Comments are closed.