LIVERPOOL YATHIBITISHA SAFARI YAKE YA AUSTRALIA

LIVERPOOL YATHIBITISHA SAFARI YAKE YA AUSTRALIA

Like
488
0
Wednesday, 04 February 2015
Slider

Klabu ya Liverpool imepanga kutembelea nchini Australia baadae mwaka huu ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kampeni ya klabu hiyo kwa mwaka 2015 hadi 2016 iliripoti klabu hiyo ya ligi ya Uingereza siku ya jumanne

Liverpool kwa mara ya mwisho ilifanya safari katika Nchi ya Australia takribani miaka miwili iliyopita

Klabu hiyo ikiwa nchini humo itacheza na klabu ya Brisbane Roar katika uwanja wa Queensland’s Suncorp tarehe 17 ya mwezi wa saba mwaka huu na baadae watacheza na klabu ya Adelaide United siku tatu mbeleni baada ya mchezo wao na Brisbane Roar

“Tulitembelea Australia kwa mara ya kwanza miaka miwili iliyopita na ushirikiano tulioupata kutoka kwa mashabiki wetu yalikuwa ya ajabu” alisema afisa mtendaji mkuu wa klabu ya Liverpool Ian Ayre kwenye maelezo yaliyotolewa na klabu hiyo

“Liverpool inazaidi ya mashabiki na wadau 600,000 Australia na tunaangalia mbele kuweza kukutana nao pindi tutakapokuwa nchini humo ”

maandalizi ni muhimu katika kujiandaa na msimu ujao wa ligi hivyo mechi kati yetu na Brisbane Roar na Adelaide United ni sehemu ya maandalizi lakini pia tunawapa nafasi wapenzi wa klabu hii kuungana na timu yao bila kujali kuna umbali gani kutoka Anfield na mahali walipo

Comments are closed.