LOUIS VAN GAAL ATANGAZA KUSTAAFU ATAKAPOMALIZA KUITUMIKIA MANCHESTER UNITED

LOUIS VAN GAAL ATANGAZA KUSTAAFU ATAKAPOMALIZA KUITUMIKIA MANCHESTER UNITED

Like
307
0
Friday, 20 March 2015
Slider

Meneja wa klabu ya Manchester United Louis van Gaal ametangaza kustaafu soka atakapomaliza kuitumikia Man U.

Meneja huyo mwenye umri wa miaka 63 anamkataba wa kuinoa Manchester United hadi mwaka 2007 baada ya kujiunga na klabu hiyo kwenye msimu wa kiangazi.

Van Gaal ambae ni raia wa Uholanzi amesema hanampango wa kuendelea na fani hiyo kwani anahitaji kuutumia muda wake na familia yake

Kocha huyu amewahi kuzinoa timu kadhaa barani Ulaya ikiwemo Barcelona, Bayern Munich na Ajax

Akizungumza kwenye mahojiano yake na daily Telegraph Van Gaal amesema umri wake umekwenda na kuinoa Man U ndio kazi yake ya mwisho kwani anahitaji kukaa na wajukuu, mke wake pamoja na watoto pia. Kocha huyo amedai hapendi hali yake ya sasa kuwa mbali na familia yake na kutolea mfano wa kushindwa kuhudhulia kwenye kumbukumbu ya kuzaliwa ya mjukuu wake.

Preston North End FC vs Manchester United FC spt_ai_manutd_valencia_14.jpg / Football - Manchester United v Valencia

Comments are closed.