LOUIS VAN GAAL: TUPO TAYARI KUPAMBANA

LOUIS VAN GAAL: TUPO TAYARI KUPAMBANA

Like
281
0
Monday, 21 September 2015
Slider

Meneja wa klabu ya Manchester United,Louis van Gaal amesema kwamba klabu hiyo ina uwezo wa kupambana kunyakua taji la Premier League.

Ushindi wa Manchester United dhidi ya Southampton umethibitisha kuwa tunauwezo wa kuchuana vikali kutwaa taji la ligi kuu, Alisema meneja Louis van Gaal.

Kikosi cha Man U chini ya Mholanzi van Gaal siku ya jumapili kilifanikiwa kuitandika klabu ya Southampton 3-2 katika uwanja wa St Mary huku mshambuliaji wake mwenye miaka 19 Anthony Martial akiiandikia klabu hiyo magoli mawili

 

Ushindi huu umeisogeza Manchester United nafasi ya pili katika msimamo wa ligi wakiwa nyuma ya wapinzani wao Manchester City ambao walilazimika kupokea kichapo cha magoli 2-1 katika uwanja wao wa nyumbani dhidi ya West Ham siku ya jumamosi

Comments are closed.