LOWASSA ATEMBELEA KARIAKOO, POLISI WATUMIA MABOMU YA MACHOZI KUTAWANYA WAFUASI WA UKAWA

LOWASSA ATEMBELEA KARIAKOO, POLISI WATUMIA MABOMU YA MACHOZI KUTAWANYA WAFUASI WA UKAWA

Like
244
0
Tuesday, 25 August 2015
Local News

JESHI la polisi mkoa wa kipolisi Ilala limelazimika kutumia mabomu ya machozi ili kuwatawanya wafuasi wa vyama vinavyounda umoja wa Katiba ya wananchi-UKAWA– kutokana na mgombea wa nafasi ya Urais kupitia umoja huo Edward Lowasa kufika eneo la kariakoo kwa lengo la kutaka kuwaona wafanyabiashara wa soko hilo.

Lowasa amefanya ziara leo ya kutembelea baadhi ya maeneo ya Jiji la Dar es salaam ikiwemo Tandale, Tandika na Kariakoo ili kutathimini hali ya maisha ya wananchi.

Kamanda wa polisi Ilala Lucas Mkondya amesema kuwa wametumia mabomu hayo kuwatawanya wafuasi kwani msafara huo unaweza kusababisha uharibifu wa mali na kuhatarisha maisha ya watu na kwamba Jeshi hilo halikuwa na taarifa rasmi ya kuwepo kwa msafara huo.

Comments are closed.