LUBANGA NA KATANGA WAREJESHWA CONGO

LUBANGA NA KATANGA WAREJESHWA CONGO

Like
175
0
Monday, 21 December 2015
Global News

MAHAKAMA ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC, imewarejesha nchini Kongo waasi wawili, Thomas Lubanga na Gemain Katanga ili waweze kutumikia vifungo vyao nchini humo.

Lubanga alishtakiwa na mahakama hiyo kutokana na makosa ya kuwa ajiri watoto wadogo katika kundi lake la waasi na kusababisha mauaji na vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu kati ya mwaka 2002 na 2003.

Germain Katanga yeye anayedaiwa kuongoza kundi lililofanya mauaji ya zaidi ya watu Elfu 2, katika wilaya ya Ituri Mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Comments are closed.