LUDOVICK UTOUH AKABIDHIWA TUZO YA UADILIFU

LUDOVICK UTOUH AKABIDHIWA TUZO YA UADILIFU

Like
297
0
Tuesday, 23 December 2014
Local News

MKAGUZI MKUU Mstaafu wa Hesabu za Serikali- LUDOVICK UTOUH amekabidhiwa tuzo ya Uadilifu na kampuni ya Dream Success Enterprises ikiwa na lengo la kutambua na kuuenzi uadilifu na utedaji kazi wake aliouonyesha katika jamii na Taifa kwa ujumla.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam Afisa Mipango na Mikakati kutoka kwenye kampuni hiyo JOSHUA LAWRENCE amesema kuwa kwa miaka 8 iliyopita hadi bwana UTOUH alipostaafu, Ofisi yaT aifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali- NAOT mpaka sasa imekuwa na mafanikio makubwa kwenye uimarishaji wa mifumo ya ukaguzi na mawasiliano kati ya ofisi yaTaifa ya ukaguzi na wadau wake.

Amefafanua kuwa kutoka na uwajibikaji na weledi bora wa kazi aliouonyesha katika kipindi chote cha kazi aliweza pia kupata nafasi ya kuteuliwa kuingia kwenye bodi ya ukaguzi ya umoja wa Mataifa –UNBOA na kuipa heshima kubwa ofisi ya Taifa ya ukaguzi naTaifa kwa ujumla.

Comments are closed.