LUTENI JENERALI KARENZI KARAKE AREJEA RWANDA

LUTENI JENERALI KARENZI KARAKE AREJEA RWANDA

Like
218
0
Friday, 14 August 2015
Global News

MIEZI miwili baada ya kukamatwa na kuzuiliwa nchini Uingereza mkuu wa ujasusi wa Rwanda Luteni Jenerali Karenzi Karake hatimaye amerejea nchini Rwanda jana.

Kiongozi huyo alikamatwa Uingereza mwezi Juni mwaka huu baada ya kukamilisha ziara ya kikazi nchini humo kwa tuhuma za uhalifu wa kivita.

Jenerali Karenzi ni mmoja wa maafisa 40 wa jeshi la Rwanda ambao majina yao yapo kwenye waranti uliotolewa na jaji wa Uhispania kutaka wakamatwe kutokana na tuhuma za uhalifu wa kivita wakati wa mauaji ya  kimbari  nchini Rwanda mwaka1994.

 

Comments are closed.