MAADHIMISHO YA KILELE CHA WIKI YA VIZIWI DUNIANI KUFANYIKA SEPTEMBA 27

MAADHIMISHO YA KILELE CHA WIKI YA VIZIWI DUNIANI KUFANYIKA SEPTEMBA 27

Like
295
0
Tuesday, 22 September 2015
Local News

WAZIRI wa Afya na ustawi wa jamii dokta Seif Rashid anatarajia kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya kilele cha wiki ya viziwi duniani itakayofanyika Septemba 27 mwaka huu kwenye viwanja vya Bwawani mjini Kibaha mkoani Pwani.

Hayo yamesemwa na Afisa Jinsia na Maendeleo kutoka Chama cha Viziwi Tanzania (CHAVITA) Lupi Mwaisaka Maswanya alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam.

Mwaisaka amesema kuwa lengo la maadhimisho hayo ni kujenga mwamko wa jamii kuhusu haki za viziwi hususani utambuzi rasmi wa lugha ya alama kama njia ya mawasiliano kwa viziwi na nafasi ya watoto wa kundi hilo katika maendeleo yao kielimu na kukuza vipaji.

Comments are closed.