MAADHIMISHO YA SIKU YA UKIMWI DUNIANI

MAADHIMISHO YA SIKU YA UKIMWI DUNIANI

Like
292
0
Tuesday, 01 December 2015
Local News

WATANZANIA leo wanaungana na watu wote duniania kuadhimisha siku ya Ukimwi ikiwa ni sehemu ya kupanua ufahamu kuhusu maafa yanayoletwa na ugonjwa huo.

 

Kama ilivyo katika maadhimisho ya Uhuru, Maadhimisho ya leo hayatafanyika kama ilivyozoeleka na badala yake fedha ambazo zingetumika katika siku hiyo zitatumika kununulia dawa za kupunguza makali ya Ukimwi- ARV.

 

Hatua hii inafuatia Agizo lililotolewa hivi karibuni na rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli ambapo Katika uamuzi wake baada ya kusitisha maadhimisho hayo, Serikali imeagiza fedha zilizotengwa kwa shughuli hiyo zielekezwe kwenye ununuzi wa dawa za kudhibiti ugonjwa huo pamoja na vitenganishi.

Comments are closed.