MAAFISA WA UHOLANZI WAFANYIA UCHUNGUZI KUANGUSHWA KWA NDEGE YA MALAYSIA MH17

MAAFISA WA UHOLANZI WAFANYIA UCHUNGUZI KUANGUSHWA KWA NDEGE YA MALAYSIA MH17

Like
214
0
Wednesday, 12 August 2015
Global News

MAAFISA wa Uholanzi wanaochunguza kuangushwa kwa ndege ya Malaysia yenye nambari ya safari MH17, wametangaza kwamba wamepata kitu ambacho kinaweza kuwa kipande cha roketi aina ya BUK inayotengenezwa na Urusi, katika eneo ilikoanguka ndege hiyo Mashariki mwa Ukraine.

Tangazo hilo lililotolewa jana ni la kwanza kutoka kwa maafisa hao, linalohusisha ushahidi wa matumizi ya roketi katika kuangushwa ndege hiyo.

MH17 iliangushwa tarehe 17 Julai mwaka jana katika eneo la Mashariki mwa Ukraine eneo linalokumbwa na mzozo, na kuuwa watu wote 298 waliokuwa ndani yake.

Comments are closed.