Maambukizi ya Ukimwi yapungua nchini

Maambukizi ya Ukimwi yapungua nchini

Like
673
0
Monday, 15 April 2019
Local News

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Uratibu, Ajira, Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama amesema kuwa utafiti wa viashiria na matokeo ya Ukimwi wa mwaka 2016/17 unaonyesha kwamba kiwango cha maambukizi ya VVU yamepungua kwa asilimia moja kutoka asilimia 5.1 mwaka  2011/2012 mpaka asilimia 5.0 kwa mwaka 2016/17.

Waziri Mhagama amesema hayo wakati akizindua utafiti huo ambapo ameeleza kuwa unaonyesha kwamba kiwango cha maambukizi ya VVU kwa watu wenye umri wa miaka 15-64 umepungua kwa asilimia moja kutoka asilimia 5.1 mwaka 2011/2012 na kufikia  asilimia 5.0 kwa mwaka 2016-2017 ambapo wanawake ni asilimia 6.5 na wanaume ni asilimia 3.5.

Amesema asilimia 60.9 ya watu wanaoishi na VVU ndio wanaofahamu hali zao ikiwa ni chini ya kiwango cha lengo ambapo amedai wamaofahamu hali zao asilimia 93.6 ndio wanaopatiwa dawa  za kufubaza makali ya VVU (ARV) ambao miongoni mwao asilimia 87.0 virusi vyao vimefubazwa.

Ameongeza kuwa utafiti huo unaonesha zaidi ya nusu milioni ya watu wanaoishi na VVU Tanzania hawajui hali yao ya maambukizi.

“Juhudi za pamoja za wenye wigo mpana zinahitajika kuwafikia watu wanaishi na VVU ambao bado hawajapima na kujua hali zao  nakuanza dawa,” alisema.

Amesema takribani watu 72,000 wanapata maambukizi mapya huku kiwango cha wanaume kujua maambukizi kikiwa kipo chini kuliko wanawake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *