MAANDAMANO NA MILIPUKO YATAWALA CONGO BRAZZAVILLE

MAANDAMANO NA MILIPUKO YATAWALA CONGO BRAZZAVILLE

Like
204
0
Tuesday, 20 October 2015
Global News

Milipuko imesikika katika mji mkuu wa Congo, Brazzaville kufuatia maandamano makubwa yaliyoitishwa na vyama vya upinzani kupinga hatua ya rais aliyeko madarakani Denis Sassou Nguesso kutaka kubadilisha katiba ili kumruhusu kuwania muhula wa tatu.

Vyama vya upinzani viliitisha maandamano hayo na inasemekana kuwa wanajaribu kuingia katikati mwa jiji hilo la Brazzaville.

Serikali ilikuwa imepiga marufuku maandamano yoyote kabla ya kura ya maoni itakayoamua iwapo katiba ya taifa hilo itabadilishwa au haitabadilishwa.

Comments are closed.