MABADILIKO YA KIUCHUMI YAIFANYA TANZANIA IPIGE HATUA

MABADILIKO YA KIUCHUMI YAIFANYA TANZANIA IPIGE HATUA

Like
292
0
Thursday, 10 March 2016
Global News

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema mabadiliko ya kiuchumi yaliyofanyika nchini yameifanya Tanzania ipige hatua kubwa katika kipindi cha miaka 10 iliyopita.

 

Ametoa kauli hiyo jana jioni wakati akihutubia kongamano la biashara baina ya Tanzania na Vietnam lililofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Kisoshalisti ya Vietnam, Bw. Troung Tan Sang.

 

Akizungumza kwa niaba ya Rais, Dk. John Pombe Magufuli, Waziri Mkuu alisema mbali ya mabadiliko ya kiuchumi, Tanzania pia imefanya mabadiliko kwenye sheria, mifumo ya kifedha na sekta za kuhudumia jamii za umma.

Comments are closed.